Peoples' Health Movement logo
Medact
We the People logo
#stopEACOP
Muhuri – Utetzi Wa Haki
Tipping Point
Racism Xenophobia Discrimination & Health

Mahakama ya Afya ya Watu – Hukumu

Mahakama ya Afya ya Watu: Uamuzi

Muhtasari

Kufuatia miezi kadhaa ya maandalizi ya kuweka kumbukumbu za vitendo vya ukatili vya Shell na Total, jamii kutoka Uganda, Msumbiji, Delta ya Niger na Afrika Kusini ziliwasilisha Mahakama ya Afya ya Watu kesi 12 ambazo zilielezea upana mkubwa wa vurugu zilizosababishwa na Shell na Total, na kuandikwa chini na serikali za kitaifa, mashirika ya kimataifa na watendaji wengine wasio wa serikali. Uamuzi huo unathibitisha kwamba mashtaka kama yalivyoorodheshwa hapa ni baadhi ya ukatili unaoendelea katika maeneo haya na zaidi. 

Kwa upana, ushuhuda uliotolewa katika tovuti zote ambapo Shell na Total zinafanya kazi pamoja kwenye mada kadhaa muhimu: uhamishaji wa lazima, uchafuzi wa mazingira (haswa wa hewa, vianzo vya maji na mchaanga/udongo), hali sugu ya afya, kiwewe, vitisho na uhalifu. Akaunti zote pia zinaonyesha kwa usumbufu kampuni hizi zikiteka nyara mamlaka ya serikali, inayotumiwa mara kwa mara ili kuamrisha yaliyo hapo juu kupitia vurugu pamoja na mauaji

Shell

Kampuni ya Royal Dutch Shell inashtumiwa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za kimazingira na kimataifa katika Delta ya Niger na Afrika Kusini. Katika Delta ya Niger, Shell pamoja na Chevron imekua ikichimba nishati ya mafuta tangu miaka ya 1950 na kusababisha madhara makubwa ya kimazingira ikiwa ni pamoja na umwagikaji mbaya wa mafuta, kuwaka kwa gesi hatari na kuenea kwa uchafuzi wa maji.1 Matendo haya mabaya yanatishia afya ya viumbe hai na wote ndani ya mfumo wa ikolojia na mfummo ikolojia wenyewe na yamesababisha mateso makubwa kwa jamii zilizoathirika.

Tulisikiliza ushuhuda zikiangazia uchafuzi wa maji na kushuhudia mafuta yakitolewa kwenye visima vya maji. Shell ilikataa kutoa tathmini za athari licha ya madai ya jamii. Kupuuzwa huku kumesababisha njaa na umaskini huku udongo ukipoteza tutuba na kutoendeleza tena jamii. Jamii ya Obelle imekabiliwa na ongezeko la visa vya saratani, kuharibika kwa mafigo, magonjwa ya moyo, matatizo ya kupumua na utasa.

Tulisikia jinsi jamii zinavyopumua hewa yenye sumu na kukabiliana na ‘hofu ya uwezekano wa milipuko ya moto’ na hatari za kaboni. Wanaotoa ushuhuda walifichua jinsi wanafamilia wanakabiliwa na kifafa, uavyaji mimba wa papo hapo, muwasho wa macho, kuungua kwa joto, kuwashwa kwa ngozi na matatizo ya kupumua. Haya yote huku maisha ya watu yakiharibiwa, na mifugo na miti kufa.

Mafuriko, yakichochewa na mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na utafutaji na unyonyaji wa mafuta bila kujali yanaongezeka nchini Nigeria. Mnamo mwaka 2022, zaidi ya watu 600 waliuawa na watu milioni 1.3 kukosa makaazi. Jamii za Niger Delta zilizama, nyumba zilizama na kuharibiwa , mashamba yalisombwa na maji pamoja na maisha ya watu. Watu wamwkwama katika kambi za wakimbiza wa ndani katika hali mbaya na msaada mdogo.

Upinzani dhidi ya Shell umekabiliwa na vurugu. Katika onyesho kubwa la kutojali maisha ya binadamu, Shell ilishtumiwa katika miaka ya 1990 kwa kushirikiana na jeshi la Nigeria na kusababisha kuuliwa kwa Ken Saro Wiwa, mwanaharakati wa mazingira na watu wengine wasio na hatia. Tulisikiliza ushuhuda kutoka jamii ya Umuechem ambao mwaka 1990 waliamua kupinga unyonyaji wa Shell. Waliitisha mazungumzo na meneja wa mkoa kupitia maandamano ya amani. Hii ilifuatiwa na polisi ‘waliojihami kwa lolote’ kufanya ‘oparesheni ya kufyatua risasi’ huku watu wakikimbia – ‘hadi vijana 50 walipoteza maisha wakati wakitorokea vichakani siku hio;kupigwa risasi kwa siasa za mafuta.’

Licha ya mazingira haya ya ukandamizaji, mashirika ya ndani ikiwa ni pamoja na We the People Nigeria, Health of Mother Earth Foundation (HOMEF), the Movement for the Survival of the Ogoni People (MOSOP), na Environmental Rights Action (ERA), wamepigana kwa ujasiri dhidi ya vurugu za uchimbaji wa miradi hii ya mafuta.

Nchini Afrika Kusini, Shell haijaonyesha kutojali sawia kwa mazingira pekee, lakini pia kwa urithi wa kitamaduni wa kiasili. Uvumbuzi wake uliokuwa umepangwa kwenye bahari kwa kutumia mawimbi haribifu ya tetemeko ulisitishwa na mahakama ya Afrika Kusini kufuatia maandamano  ya makundi ya wenyeji. Upelelezi uliopangwa wa Shell katika Pwani ya Pori ni tishio kwa afya ya watu wanaoishi katika jamii, ambao bahari sio tu chanzo cha chakula inayovurugwa kwa urahisi na shughuli za uchimbaji, lakini chanzo cha uhusiano wa kina wa kiroho.

Athari za kiafya za sera za uziduaji katika dhamana takatifu kati ya watu na mazingira ambayo inawadumisha hazijaonyeshwa kwa urahisi katika mifano ya kisasa ya matibabu, lakini mataifa ya kiasili kote ulimwenguni yamesisitiza mara kwa mara juu ya matokeo mabaya juu ya ustawi wa watu katika jamii wakati ushirika na ardhi umevurugwa au kupotoshwa.

Watu wa Xhosa pamoja na vikundi kama vile Kamati ya Mgogoro wa Amadiba na jamii ya Mpondo, wameonyesha ujasiri wa ajabu, wakipigania kuhifadhi mazingira yao na Maisha yao. Licha ya kukabiliwa na vitisho na vurugu, upinzani wao umesababisha ushindi mkubwa, kama vile ubatilisho wa hapo awali wa leseni ya utafutaji ya Shell Afrika kusini. Walishinda kabla na watashinda tena!

Total

TotalEnergies kwa sasa inahusika katika kutatiza sana ukiukwaji wa haki za mazingira na haki za binadamu nchini Uganda na Msumbiji. Nchini Uganda, Total inaongoza kwa utengenezaji wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), ambalo litasafirisha mafuta ghafi katika umbali wa kilomita 1,400 kutoka Uganda hadi Tanzania. Njia iliyopendekezwa ya EACOP inavuka mifumo nyeti ya ikolojia na ardhi asilia, na hivyo kusababisha hatari kubwa kwa kilimo cha ndani, viwanda vya uvuvi na afya ya jamii. Ni dhahiri kwamba, utoaji wa Notisi za Umiliki wa Ardhi wa serikali ya Uganda mwaka 2019 umesababisha takriban kaya 14,000 kuhama makazi yao, jambo linalosisitiza gharama kubwa za kibinadamu na kitamaduni za mradi huu.

Kutoka Uganda, tulisikiliza shuhuda za kuhamishwa, kupokonywa ardhi, vitisho, kupoteza maisha na kuzorota kwa afya. Familia na jamii zimehamishwa kutoka kwa nyumba za mababu zao bila kulipwa fidia. Maisha ya watu yameharibiwa kwa kuhamishwa, na kusababisha familia kupata shida kulipa karo yoyote ya shule, mahitaji ya kimsingi, kupata huduma za afya na dawa. Upotevu wa ardhi umesababisha ‘kuenea kwa njaa, umaskini na kuvunjika kwa familia’.

Licha ya changamoto zinazoendelea za kisheria na upinzani mkubwa, Total ilitangaza mnamo 2022 uamuzi wao wa kuendelea na ujenzi. Total ilikuja na ahadi za kuboresha viwango vya maisha lakini pamoja na maendeleo ya EACOP, lakini badala yake, watoa ushuhuda walishiriki jinsi “hatuna ardhi na ni maskini zaidi nchini”. Kama shuhuda zilivyotolewa, juhudi za upinzani, zinazoongozwa na kampeni ya StopEACOP, mara nyingi hukabiliana na vurugu na vitisho.

Nchini Msumbiji, Total imezindua mradi ambao utatoa kiwango cha gesi ya methane ambacho kitaongeza uzalishaji wa gesi chafuzi katika nchi nzima kwa hadi 14%, katika nchi ambayo tayari iko katika hatari kubwa ya mabadiliko ya hali ya hewa. Ubia wa Total nchini Msumbiji umekuwa na unyonyaji na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu wa kimataifa. Harakati za kampuni ya kuchimba gesi asilia yenye futi za ujazo trilioni 65 ifikapo mwaka 2024 zimejaa hatari za kijamii na kiuchumi, haswa ikizingatiwa hali ya kutokuwa na utulivu inayoendelea mkoa huo, ambayo imechangiwa na “Kashfa ya Tuna Bond” mnamo mwaka 2016 na kusababisha mzozo wa kiuchumi.

Kuongezea dhiki hiyo, ujenzi wa hifadhi ya gesi asilia ya Afungi Liquified Natural Gas umesababisha kaya 557 kuondolewa kwa nguvu. Jamii za wavuvi ambao walikuwa wakiishi sio mbali kutoka baharini kwa vizazi kadhaa walihamishwa hadi kwenye “kijiji cha kuhamishwa” zaidi ya kilomita 10 ndani, bila njia ya kufikia bahari. Wakulima ambao sasa walikuwa wamepoteza ardhi yao, walipewa vipande vidogo vya ardhi visivyotosheleza mbali na nyumba za uhamisho walizohamishiwa. Kutokana na hali hiyo, jamii hizo zimepoteza maisha na kuachwa maskini.

TotalEnergies, kama sehemu ya kiwanda cha gesi, imehusishwa na mzozo mkali kati ya waasi, vikosi vya jeshi na mamluki. Kufikia sasa, mzozo huu umehamisha watu milioni 1, na pia kusababisha unyang’anyi, utekaji nyara, vitisho kwa familia, unyanyasaji wa kijinsia, na kwingineko.

Kufuatia shambulio kubwa la waasi kwenye kijiji cha Palma—kijiji kikubwa cha karibu zaidi na Hifadhi ya Afungi—mnamo Machi 2021, TotalEnergies ilitelekeza eneo hilo na michakato inayoendelea na jamii, ikidai ‘force majeure’. Walisitisha mradi kwa muda usiojulikana, wakisimamisha malipo yote ya fidia. Katika kuongeza mapato kupitia kampuni tanzu katika maeneo ya kodi, TotalEnergies pia imeepuka kulipa kodi kubwa nchini.2 Wakati huo huo, shughuli zake zimesababisha athari mbaya za kiuchumi kwa jamii.

Kesi zote zinaangazia dharau ya TotalEnergies kwa mazingira na haki za binadamu za kimataifa katika harakati zao za kupata faida. Vitendo vya kampuni hiyo vimesababisha uharibifu mkubwa wa ikolojia, kuhamisha maelfu ya wakaazi wa eneo hilo, na vinahusishwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu za kimataifa.3

Kanuni zinazoongoza

Utaratibu huu unajitambua na kujiweka ndani ya historia pana ya kupanga na upinzani dhidi ya dondoo duniani kote.

1. Uwajibikaji kwa jamii zilizoathirika

Uamuzi huu na mchakato ni wa kwanza kabisa kuwajibika kwa jamii zilizoathirika, ambazo zimetoa ushuhuda. Tunatambua kuwa huu ni mchakato wa moja kwa moja, badala ya tukio ambalo linaweza kutengwa na kuchunguzwa. Uamuzi huo unajengwa juu ya uzoefu wa majaji na kwa uwazi katika mazungumzo na jamii zilizoshiriki katika mahakama hiyo.

2. Afya

Afya inaeleweka kwa maana yake pana zaidi. Hii ina maana kwamba afya si tu hali kamili ya ustawi wa kimwili, kiakili, kijamii kama inavyomhusu mtu binafsi, bali ni ya pamoja, kiikolojia, kitamaduni na kiroho. Kuanzia hapa, tunathibitisha haki ya wote kwa afya kama hiyo.

3. Ardhi, lugha, ukombozi

Tunaongozwa na mazoea na nakala za ukombozi za watu wa kiasili, walio na ardhi na maji, na kuthibitisha uhusiano wa kina wa watu hawa na haki ya kujiamulia ardhi za mababu zao, ambapo tamaduni na lugha zao pia hutoka.

4. Mapungufu ya mifumo ya kimataifa

Tunashutumu viwango viwili vya hali ya kimataifa iliyojengwa juu ya ukandamizaji unaoendelea na mauaji ya halaiki ya watu wa asili ya Kiafrika. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, likitumia uwezo wake wa kura ya turufu usio na uwiano, linafichua mfumo huu wa ngazi mbili katika kutofautiana kati ya sera na matendo yake. Tofauti hii imeainishwa katika Jopo la Ngazi ya Juu ya Vitisho, Changamoto na Mabadiliko (2004) na inathibitishwa zaidi na kutokuwepo kwa utaratibu halisi wa kimataifa unaofanya kazi – kisheria au vinginevyo – kuwajibisha serikali na taasisi.

5. Kuvunja mifumo ilio na nguvu katika utawala

Tunakubali uimarishaji wa matriki ya nguvu ya hegemonic ambayo hueneza itikadi za uchimbaji na utawala kati ya desturi za Shell na Total – yaani ubepari wa rangi ya kikoloni na uwezo wa cis-heteropatriaki – na haja ya kusambaratisha mifumo hii.

6. Mifumo mipya ya kutengeneza ulimwengu

Tunatambua na kukaa katika mvutano kati ya kanuni za ujenzi kwa mustakabali uliokombolewa kwa pamoja huku tukipanga mikakati ya kubadilisha hali halisi tuliyo nayo sasa. Tunaongozwa na usawa wa haya. Hii ni pamoja na kutambua mapungufu ya ‘demokrasia’ ya uchaguzi na mfumo wa ‘haki’ ya jinai – na kushindwa kwao kutoa haki yoyote ya maana. Tunaheshimu na kushikilia maono hayo ya ulimwengu ambapo mashirika kama Shell na Total hayapo tena. Kukamilishwa kwa mchakato kamili wa fidia ulioainishwa hapa chini kunaweza kusababisha mwisho wa kuwepo kwa Shell na Total kama huluki.

Uamuzi

Kwa vitendo vilivyotajwa hapo juu, tunaona Shell – inawajibika kupitia bodi zake za wakurugenzi za awali na za sasa – ikiwa na hatia kwa shughuli zake katika Delta ya Niger na Afrika Kusini, ambayo tunaona kuwa na madhara makubwa kwa maisha, afya, haki ya makazi, ubora wa maisha, haki ya kuishi kwa utu, ubora wa mazingira, haki ya kuishi bila ubaguzi na ukandamizaji, haki ya maji safi na haki ya kujitawala kwa jamii zilizoathiriwa.

Kwa vitendo vilivyotajwa hapo juu, tunaona TotalEnergies ina hatia kwa shughuli zake nchini Msumbiji na Uganda, ambazo tunaziona kuwa na madhara makubwa kwa maisha, afya, haki ya makazi, ubora wa maisha, ubora wa mazingira, haki ya kuishi bila kubaguliwa na ukandamizaji, haki ya maji safi, na haki ya kujitawala kwa jamii zilizoathiriwa.

Tunazipata Serikali za Uingereza, Uholanzi na Ufaransa na hatia kwa kuunga mkono na kuendeleza uwekezaji na uchimbaji unaodhuru na usiowajibika wa mafuta na gesi katika Jangwa la Sahara la Afrika.

Tunapata serikali za Msumbiji, Afrika Kusini, Uganda, na Nigeria na hatia ya kutowajibika kwa kushindwa kuanzisha na kutekeleza sheria, kanuni, na ufuatiliaji na utekelezaji ili kulinda haki za watu wake.

Pia tunapata taasisi kama vile Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, Benki ya Dunia na Shirika la Biashara Ulimwenguni ambazo zinaunda usanifu wa kimataifa wa kifedha na hatia ya kuunda mazingira, kupitia sera na mazoea yake, ambayo yanahatarisha uhuru wa kiuchumi wa mataifa na familia ambazo zimetawaliwa. zilizojawa na ada za shule, kwa mfano, kutokana na programu za marekebisho ya kimuundo, Mkataba wa Nishati na Usuluhishi wa Migogoro ya Nchi ya Wawekezaji.

Tunapendekeza kwamba mauaji makubwa ya moja kwa moja na ya kijamii ya utaratibu – iwe kwa njia ya ghasia za kijeshi na za kijeshi (kama inavyotolewa katika shuhuda kutoka Msumbiji), athari mbaya za kiafya za vitendo vya uchimbaji (kama vile uchafuzi wa vyanzo vya maji vilivyoangaziwa katika shuhuda kutoka Ogoniland, Niger Delta) au athari za chini za mkondo kwa hali mbaya ya hewa (kama vile mafuriko, yaliyoelezwa tena katika Delta ya Niger) yanajumuisha mauaji ya kimbari yenye ufanisi,4 pamoja na mauaji ya ikolojia.

Madai/mapendekezo

Madai kwa Shell na Total

WACHA
  1. Mipango yote amilifu ya upanuzi wa tovuti zilizopo za uchimbaji wa mafuta, na kuweka usitishaji wa kudumu wa utafutaji wa tovuti mpya.
  2. Kushirikiana na kufadhili majeshi na vikundi vya kijeshi, na kutumwa kwa vikosi vya usalama vya kibinafsi katika unyanyasaji kwa jamii za mitaa, na kuhakikisha kutorudiwa kwa hili katika siku zijazo.
ANZA

Kuunda miundombinu kwa ajili ya mchakato wa haki ya urekebishji

  • Tunadai kukiri hadharani kwa hatia na kuanza kwa mchakato wa haki ya urekebishaji. Jamii zilizoathiriwa lazima ziongoze juu ya nini haswa hii inajumuisha. Mapendekezo ya muda ni pamoja na:
    • Vikao vya upatanishi vya papo hapo na jamii zilizoathirika kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya haki. Mashirika kulipa ada zote, hakikisha upatanishi unapatikana katika lugha za Wenyeji na kuandika mchakato huo. Upatanishi unaongozwa na jamii zilizoathiriwa na waangalizi wa kimataifa waliochaguliwa na jamii hizi, na madai ya wazi ya jinsi ya kuendelea.
    • Tokeo moja linaweza kuwa hukumu la Watu la bodi ya wakurugenzi wa makampuni na maafisa husika wa serikali ya Uingereza/Ufaransa.

Kusaidia hatua ya mbele kwa haki ya afya kwa jamii

  1. Kufadhili ukaguzi huru wa afya kwa muda mrefu (yaani kwa vizazi kadhaa) katika jamii zilizoathiriwa ili kuweka ramani ya athari za kiafya za uchimbaji wa mafuta.
  2. Fidia ya maana ya kifedha, ikisubiri ukaguzi wa rekodi za fedha kwa uamuzi wa viwango vya mwisho vya adhabu kwa kila jamii.
  3. Ufikiaji unaohitajika na usiojulikana wa huduma ya afya ya dharura na ya muda mrefu kwa wale wote wanaoishi na/au wanaofanya kazi katika eneo la uchimbaji wa mafuta ya visukuku – bila mzigo wa uthibitisho kwa jamii kuonyesha hali mbaya ya afya kama inavyohusishwa na uchimbaji wa mafuta.
  4. Kufadhili miundomsingi ya utafiti wa umma ili kukusanya data ya janga la kijamii kuhusu athari za uchimbaji wa mafuta.

Kurekebisha athari za uhamishaji wa kulazimishwa

  1. Ambapo jamii zimehamishwa lakini hakuna ujenzi wa miundombinu ya uziduaji ulioanza, ardhi yao na rasilimali zinazohusika hurejeshwa mara moja.
  2. Pale ambapo urejeshaji wa papo hapo hauwezekani kwa sababu ya uchimbaji unaoendelea wa mafuta ya visukuku na athari zake zinazohusiana, kuna fidia ya kutosha kwa ajili ya kupoteza makazi, ardhi, riziki na kusababisha majeraha na afya mbaya, pamoja na utoaji usiojulikana wa makazi salama, ya hali nzuri.

Kusafisha na kurekebisha maeneo ikiwa ni pamoja na hewa iliyoathirika, maji na ardhi

  1. Kufadhili tathmini kali na huru ya athari za mazingira na kiafya na data zote zinazopatikana kwa uhuru na hadharani.
  2. Miundombinu ya mafuta iliyopo lazima ivunjwe na kuondolewa kwa usalama, hivyo basi kupunguza madhara zaidi ya kiikolojia.
  3. Usafishaji lazima uzingatie viwango vya ubora wa mazingira vya kimataifa au vya kampuni ya nchi ya nyumbani (EQS) – yoyote ambayo ina nguvu zaidi. Hii pia inajumuisha kurejesha maeneo hayo kadiri iwezekanavyo vile yalipatikana kabla ya uchimbaji.
  4. Pale inapotakiwa na wanajamii, kuna uhamisho unaogharamiwa na gharama zote kwa wale wote wanaotaka kuondoka eneo hilo kwa muda wa kusafisha na kuondoa uchafuzi, na masharti ya kurejea mara ardhi inapokuwa salama kukaa.

Kutambua mamlaka ya mitaa na kutambua mahitaji ya kampeni za mitaa

  1. Nchini Uganda, tunatoa wito kwa Total kusitisha Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kulingana na  kampeni ya StopEACOP inayoungwa mmkono ndani ya taifa na kimataifa.
  2. Katika Delta ya Niger, tunatoa wito kwa Shell kukidhi kikamilifu mahitaji yaliyotolewa katika ilani ya Niger Delta ya Haki ya Kiikolojia ya Kijamii.

Kufadhili na kushirikiana pamoja na masharti yote ya mabadiliko ya haki5

  1. Jitolee kwa haki ya nishati ya ndani kwa kipindi cha mpito kwa sheria na masharti ya jamii, na mpito wa haki kwa kazi zinazostahili na bora kwa wafanyakazi wote, kushughulikia mahitaji yao kama ilivyoainishwa katika ”Mfumo wa Mkakati wa Mpito wa Haki”. 
  2. Fidia jamii kwa athari za kiafya zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na uchimbaji wa nishati ya visukuku, kulingana na tathmini huru za hatia kama vile Wakati wa Kulipa.

Madai kwa serikali na taasisi

  1. Serikali za Uganda, Nigeria, Afrika Kusini, Msumbiji
WACHA
  1. Kutumia ushuru na ruzuku ya ardhi kupanga mifuko ya mashirika ya mafuta ambayo husababisha madhara makubwa kwa jamii.
  2. Kuidhinisha mpango wowote wa sifuri usioweka kipaumbele katika uondoaji wa nishati ya kisukuku na mpito wa haki unaohusishwa.
  3. Kuwezesha polisi na vikosi vya kijeshi kutisha na kushambulia jumuiya za mitaa kwa jina la kulinda maslahi ya mashirika ya mafuta ya mafuta au maafisa wa serikali walioshiriki.
  4. Kataza matumizi ya usalama wa kibinafsi na vikosi vya kijeshi na mashirika ya mafuta, na uhakikishe kuwa hakuna kurudia kwa vurugu.
ANZA

Kujenga miundombinu kwa ajili ya haki ya fidia

  1. Toza faini mashirika ya uzinduaji kwa madhara na uharibifu ambayo yamesababisha kwa jamii na maeneo yao kwa miongo kadhaa katika kutafuta nishati ya mafuta. Faini hizi basi zitumike kuelekea haki ya fidia kwa jamii hizi.
  2. Kubali kuwa jimbo lako katika kuwezesha vurugu za mafuta na anza mchakato wa urekebishaji wa haki kwa kufuata mwongozo wa jamii zilizoathiriwa kuhusu jinsi hali hii inavyoonekana.
  3. Lipa na uwezeshe Mazungumzo ya Kitaifa ya Maridhiano yanayoongozwa na Jamii kwa kila jamii kushiriki malalamishi na madai yao.
  4. Inapohitajika na jamii zilizoathiriwa, heshimu wito wao wa kujiuzulu kwa wawakilishi wa mawaziri, wa majimbo na wa serikali za mitaa, na kuandaa uchaguzi mpya.
  5. Pale ambapo jamii zilidai, tengeneza mbinu shirikishi za kidemokrasia kama vile hukumu ya watu kuhusu maafisa.

Marejesho ya haki za ardhi

  1. Rejesha na kulinda haki za ardhi za kiutendaji na za kisheria za watu wa kiasili na wenyeji kwa maeneo ya mababu zao kiasi kwamba hawawezi kutengwa.
  2. Maamuzi yoyote kuhusu matumizi ya ardhi lazima yafanywe na jamii ya eneo hilo.
  3. Kuhakikisha ulinzi wa watetezi wa ardhi na familia zao.

Kurejesha maeneo ikiwa ni pamoja na hewa iliyoathirika, maji na ardhi

  • Unda mahitaji ya kisera na kisheria yanayoamuru mashirika yanayochafua mazingira kuyasafisha, kubainisha muda kama ilivyokubaliwa na jamii zilizoathiriwa. Usafishaji lazima uzingatie viwango vya ubora wa mazingira vya kimataifa au viwango vya ubora vya kampuni ya nchi ya nyumbani (EQS) – yoyote ambayo ni nzuri zaidi. Hii ni pamoja na kuhakikisha mashirika yanarejesha kadiri iwezekanavyo maeneo kwa jinsi yalivyopatikana kabla ya uchimbaji.

Kuchukua hatua kuelekea katika haki ya kiafya

  1. Kufadhili tathmini huru za athari za mazingira na afya, kwa kutoza faini mashirika yanayochafua mazingira kwa shughuli zao za uziduaji.
  2. Kuanzisha miundo msingi ya utafiti wa umma ili kukusanya data ya magonjwa ya kijamii kuhusu athari za uchimbaji wa mafuta katika maeneo yaliyoathirika, yanayolipiwa na (mashirika) yanayochafua mazingira.
  3. Tambua uzito wa hitaji la kiafya na uhakikishe ufikiaji wa huduma ya afya ya papo hapo na ya muda mrefu kwa wale wote walioathiriwa na mashirika yanayochafua mazingira.

Kusimamia haki ya kubadilisha Maisha ya watu

  1. Kwa kuongozwa na matakwa ya jamii zilizoathiriwa, hakikisha mabadiliko yanaodumisha haki ya nishati kwa wote na kuwezesha mabadiliko kwa wafanyikazi wa ndani walioajiriwa katika tasnia ya mafuta.
  2. Jamii, wafanyakazi, majimbo na washikadau wengine wanahitaji kwa ushirikiano kufikia mabadiliko ambayo yanakuza ukarabati, urejeshaji, usawa, haki na manufaa ya wote. Mabadiliko ya nishati ya kijani pia yanahitaji kuhakikisha usambazaji wa haki na kipaumbele cha nishati kuhudumia mahitaji ya umma kuliko faida. 

b)  Serikali za UK, Uholanzi na Ufaransa

(nchi ambazo makampuni haya yana makao makuu au ambayo yana uhusiano nayo)

WACHA
  1. Kutumia pesa za umma kugharamia mashirika ya mafuta
  2. Kutoa leseni kwa miradi mipya ya mafuta nchini Uingereza, Uholanzi na Ufaransa
  3. Kuidhinisha mpango wowote wa “sifuri halisi” ambao hauwekei kipaumbele uondoaji wa nishati ya kisukuku na haki ya mabadiliko inayohusishwa.
  4. Kutumia nguvu za kimataifa za kisiasa na kiuchumi kusaidia mifumo ya kisheria na ya ziada ya kisheria ambayo inadumisha na kuwezesha vurugu za Shell na Total.
ANZA

Kuwajibika kwa vitendo vya Shell na Total

  1. Fidia kwa kifedha jamii za mstari wa mbele zilizoathiriwa na kushiriki katika mchakato wa haki ya ulipaji inavyotakiwa na jamii zilizoathiriwa.
  2. Agiza kila kampuni kugharamia gharama za kampeni za kimataifa za uhamasishaji (zinazoendeshwa na mashirika ya mashinani) kuhusu sera na vitendo vyao vya uziduaji.

Kutumia sheria za kitaifa kuwawajibisha Shell na Total

  • Tekeleza kisheria mapendekezo yaliyo hapo juu yanayolengwa kwa Shell na Total kwa kutumia sheria za kitaifa na kimataifa.

Kuzingatia matakwa ya vuguvugu la haki ya kufidia

  • Shiriki katika tathmini huru ya athari za ukoloni na ukoloni mamboleo kwa jamii barani Afrika, ikiongozwa na wasomi wa fidia wa Kiafrika na jamii. Hii inapaswa kujumuisha tathmini ya athari za kiafya zinazoendelea za uchimbaji wa rasilimali na shida ya hali ya hewa ambayo nchi kama vile Uingereza, Uholanzi na Ufaransa zinawajibika kwa kiasi kikubwa. Tunatazamia mahitaji ya muungano ya Fidia Uingereza (​​https://climatereparations.uk/#demands) kama hatua ya kuanzia.

Kusimamia haki ya mabadiliko ya Watu

  • Jumuiya, wafanyakazi, majimbo na washikadau wengine wanahitaji kwa ushirikiano kufikia mabadiliko ambayo yanakuza ukarabati, urejeshaji, usawa, haki na manufaa ya wote. Mabadiliko ya nishati ya kijani pia yanahitaji kuhakikisha usambazaji wa haki na kipaumbele cha nishati kuhudumia mahitaji ya umma kuliko faida.

C) Mashirika ya kimataifa

WACHA
  • Madai au tishio la kushtakiwa kwa mashirika ya mafuta, au makampuni ya nchi zilizo na makao makuu, kupitia Usuluhishi wa Migogoro ya Wawekezaji na Jimbo (ISDS) na mbinu zinazohusiana. Kuongezea, tunatoa wito mahususi wa kuondolewa kwa Mkataba wa Nishati.
ANZA

Kutambua uhalifu wa vita wa mashirika ya nishati ya mafuta, mauaji ya halaiki/kimbari na uharibifu wa mazingira

  • UN (na haswa Ofisi ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari na Wajibu wa Kulinda) kuhoji na kufafanua upya mauaji ya kimbari kama yalivyoundwa na matokeo, badala ya dhamira.

Utambuzi wa ukoloni wa walowezi wa mafuta

  • UNHCR kutambua haki za wale waliokimbia makazi yao kutokana na viwanda vya uzinduaji, chini ya neno mkimbizi wa ndani.

Uwajibikaji wa kisheria ya kimataifa wa mashirika ya mafuta

  • Anzisha kesi za kisheria chini ya mahakama ya kimataifa ya jinai dhidi ya mashirika ya mafuta na/au watendaji wao kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.6

Kuunganisha mahitaji kwa uanachama wa mashirika ya kimataifa au miungano

  • Mashirika ya kimataifa kuunganisha haki ya uanachama na wajibu wa kutimiza matakwa ya ulipaji – kwa mfano. hitaji la bajeti iliyotengwa kwa ajili ya fidia kamili kwa jamii zilizoathiriwa na athari za zamani, za sasa na zijazo zisizotarajiwa za ajenda na desturi hizi za shirika la uhalifu. Haki ya kusimamisha uanachama hadi mahitaji yatimizwe.

Mapendekezo kwa harakati

WACHA
  • Kuidhinisha ‘ubepari wa kijani’ na kuendelea uchimbaji wa kikoloni kwa nishati mbadala.
ANZA

Kukuza mshikamano wa kimataifa katika mapambano

  1. Kuza na kuimarisha uhusiano wa kusini-kusini/kusini-kaskazini kwa kujitolea kujifunza kwa kina na kujenga uwezo wa kuchukua hatua za pamoja.
  2. Unganisha kwa uwazi na upange katika mapambano yote – kutambua kuwa haya yote yanaendeshwa na mifumo sawa ya mamlaka iliyofafanuliwa hapo juu.

Kutumia njia za kawaida za uwajibikaji

  1. Tambua mawakili wanaotekeleza sheria za kimataifa ili kuendeleza kesi za hatua za ngazi ya juu dhidi ya Shell na Total kupitia Mahakama ya Kimataifa ya Jinai na/au vinginevyo.
  2. Tambua na utumie uwezo wa kuchukua hatua za wanahisa dhidi ya Shell na Total, na wale wanaozifadhili.

Kujitolea kwa upangaji wa mapendekezo

  • Ahadi hii inataka kuangaliwa upya kwa taasisi za kisiasa na mienendo wanayowajibika kwayo. Hii inamaanisha sio tu kufanya kazi kuelekea uvunjwaji wa jumla wa mifumo ya nguvu ya utawala iliyoelezwa hapo juu, lakini kuandaa kuunda mifumo ya sera na vitendo vya ‘kuthibitisha maisha’7 ambayo haiwalindi walio hatarini dhidi ya unyonyaji lakini inayozuia jamii kuwa wa kunyonywa hapo kwanza.

Vidokezo

1. UNEP Environmental assessment of Ogoniland (2011): https://wedocs.unep.org/20.500.11822/7947

2. https://thewire.in/world/oil-and-gas-multinational-total-is-making-a-mess-in-mozambique

3. Uamuzi huu unatokana na vyombo vifuatavyo vya kimataifa, kama ilivyoangaziwa na Mahakama ya awali ya Popular Internacional de Salud: Tume la Marekani la Haki na Wajibu wa Mwanadamu (1948), Mkataba wa Kimataifa wa Kiuchumi, Kijamii na Haki za Utamaduni (1966), Azimio la Alma-Ata (1977), Mkataba wa Ottawa wa Kukuza Afya wa Shirika la Afya Duniani (1986), Itifaki ya San Salvador (1988), Mkataba wa 169 wa Shirika la Kazi Duniani (1989), the Azimio la Afya ya Watu (2000), Mkataba wa Bangkok wa Kukuza Afya katika Ulimwengu wa Utandawazi (2005), na Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watu wa Kiasili (2007).

4. Ndani ya Mkataba wa 1948 wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari, ufafanuzi wa mauaji ya kimbari unawekwa kama:

“kitendo chochote kati ya zifuatazo zilizofanywa kwa nia ya kuharibu, kwa ujumla au kwa sehemu, kikundi cha kitaifa, kabila, rangi au kidini, kama vile:

1. Kuua wanachama wa kikundi;
2. Kusababisha madhara makubwa ya mwili au kiakili kwa washiriki wa kikundi;
3. Kuweka kwa makusudi hali ya maisha ya kikundi kuleta uharibifu wake wa kimwili kwa ujumla au sehemu;
4. Kuweka hatua zinazokusudiwa kuzuia kuzaa ndani ya kikundi;
5. Kuwahamisha watoto wa kikundi hicho kwa lazima kwenda kwa kikundi kingine.

Ufafanuzi huu wa mauaji ya kimbari unalazimu ‘dhamira’. Hata hivyo, tunaamini kwamba vitendo vya Shell na Total vinalingana na ujinga wa kukusudia ambao kimsingi unajumuisha nia.

5. Mfumo elekezi wa mbadiliko wa haki unaorejelewa hapa unajengwa juu ya ile iliyowekwa na Movement Generation hapa: https://movementgeneration.org/wp-content/uploads/2016/11/JT_booklet_English_SPREADs_web.pdf

6. Kwa taarifa zaidi; https://www.greenpeace.org/static/planet4-netherlands-stateless/2023/03/f9f5d5b6-inventory-of-crimes.pdf

7. Tunatoa msemo huu kimakusudi kutoka kwa kazi ya mkomeshaji magereza Dkt Ruth Wilson Gilmore.

Medact © 2022 | Registered Charity 1081097 | Company Reg No. 2267125 | The Brick Yard (formerly Grayston Centre), 28 Charles Square, London N1 6HT, UK